Virusi vya Korona vinavyozidi kubadilisha hali ya kawaida ya maisha, watu duniani kote wanatafuta maelezo kuhusu jinsi ya kukaa salama, kuwa na tumaini na kusaidiana.

Dunia inaweza kudhibiti virusi na athari zake ikiwa tu kila mtu anaweza kupata habari sahihi na za kuaminika. Verified ni hatua ya Umoja wa Mataifa inayolenga kupunguza habari zisizoaminika kwa kutoa habari unazoweza kuamini: habari za kuokoa maisha, ushauri wa kweli, na simulizi bora zaidi maishani. Angalia alama mbili zinazoashiria uthibitishaji.

Jisajili

Sababu Yetu Kuwepo

Hivi sasa unashiriki katika mradi mkubwa zaidi wa ushirikiano wa kijamii ambao dunia imewahi kushuhudia. Mkubwa kuliko kutua mwezini, kuliko Olimpiki, kuliko ujenzi wa jumba refu zaidi au daraja refu zaidi. Mabilioni ya watu wanafanya kazi kwa pamoja – daktari upande ule mwingine wa nchi. Mzazi anayemfunza mtoto nyumbani. Mwanasayansi anayeshughulikia chanjo. Muuguzi anayefanya kazi bila kupumzika. Wewe, unayesoma haya. Kujitahidi kufikia lengo moja la kijumla: kulinda kila mmoja.

Katika janga hili, kusambaza habari zinazoaminika na zilizothibitishwa kutasaidia kuweka kila mtu katika hali ya usalama, ilhali, habari potovu zinaweza kuweka maisha hatarini. Ikiwa unataka kuhakikisha kuwa habari unazosambaza zinasaidia ulimwengu, jisajili ili kupokea habari kutoka Verified, na kwa wakati wote angalia alama ya Verified.

Tunafanya haya kwa ajili ya kila mmoja – kwa kila mtu aliye kwenye timu kubwa zaidi ambayo dunia imewahi kuona.