Kuhusu

Hapajawahi kuwa na hitaji kubwa kama hili la habari sahihi, iliyothibitishwa

Ulimwengu unapokabiliana na changamoto kubwa zaidi katika inayoweza kukumbukwa na walio hai, kuna haja kubwa zaidi ya habari sahihi, iliyothibitishwa. Kama virusi vyenyewe, habari potovu huenea kutoka kwa mtu mmoja hadi mwingine, na kuongeza hatari kwa afya na kueneza hofu na mgawanyiko. Ulimwengu hauwezi kuudhibiti ugonjwa huu na athari zake bila kupatikana kwa habari zinazoaminika, sahihi na ambazo zinakuza sayansi na suluhisho halisi – na zinazokuza ushirikiano kati ya mataifa.

Verified ni hatua ya Umoja wa Mataifa, kwa kushirikiana na Purpose, ili kutoa habari za kuaminika na kuokoa maisha, ushauri wa kweli na simulizi bora za kibinadamu.

Kwa kuendeleza na kusambaza habari kutoka Verified, watu wa kawaida wanaweza kuchukua jukumu muhimu katika kazi ya Verified kwa kueneza habari za kuaminika kuhusu COVID-19 kwa rafiki zao, familia na mitandao ya kijamii, kwa lengo la kuokoa maisha na kukabiliana na habari potovu. Mashirika, biashara, asasi za kijamii na majukwaa ya vyombo vya habari yanashirikiana na Verified ili kusambaza habari zinazosaidia kulinda watu, jamii na zinazoendeleza ushirikiano duniani kote.

Timu ya wanaoshiriki habari katika Verified, wanaobuni na watafiti hutoa habari kulingana na maelezo na mwongozo wa kisasa kutoka Umoja wa Mataifa, Shirika la Afya Duniani na mashirika mengine ya UN. Tunafanya kazi na wataalam wanaoongoza kwenye Rasimu ya Kwanza ya habari potovu, na watafiti wa ukweli wanaojitegemea.

Verified inafanya kazi kwa msaada wa Luminate, IKEA Foundation na UN Foundation na washirika kote duniani.