Masharti ya Huduma
Maudhui ambayo tunaweza kutoa kupitia tovuti hii ya shirika la Verified hayakusudiwi kuchukua nafasi ya mashauriano sahihi ya mtaalamu wa huduma za afya mwenye leseni kwa uchunguzi, tiba, kupunguza, matibabu au kinga ya magonjwa, majeraha au hali zingine. Hupaswi kutegemea maudhui yoyote tunayotoa kupitia huduma hizi katika uamuzi wako wowote wa huduma ya kiafya au wa kimatibabu. Taarifa inayotolewa hapa sio ushauri wa kimatibabu.
Masharti
Verified imejitolea kulinda faragha ya wanaotembelea tovuti yetu, na mtu mwingine yeyote ambaye tunachakatia maelezo ya kibinafsi. Tunaamini kwamba uko na haki ya faragha kwenye wavuti wetu. Sera hii inaweka wazi jinsi tutakavyochukulia maelezo yako ya kibinafsi.
1. Sisi ni kina nani?
Kwa madhumuni ya kufuata sheria, shirika ambalo linakusanya data yako ni Verified, Purpose Global PBC, 115 5th Avenue, 6th Floor, New York, NY 10003. Unaweza kuwasiliana nasi kupitia hello@shareverified.com wakati wowote.
2. Je, tunakusanya maelezo gani?
Tunaweza kukusanya, kuhifadhi na kutumia aina zifuatazo za data ya kibinafsi:
- Maelezo kuhusu kompyuta yako na vile unavyotembelea na kutumia tovuti hii ikijumuisha anwani yako ya IP, eneo la kijiografia, aina ya kivinjari, chanzo cha rufaa, urefu wa muda wa kutembelea tovuti na idadi ya maoni ya ukurasa.
- Maelezo yanayohusiana na miamala inayotekelezwa kati yako na sisi kuhusiana na tovuti hii, ikijumuisha maelezo yanayohusiana na mchango wowote unaofanya kwetu.
- Maelezo unayotoa kwetu kwa madhumuni ya kujiandikisha kwetu k.m. anwani yako ya barua pepe na maelezo mengine ya kibinafsi unapojisajili.
- Maelezo unayotoa kwetu kwa madhumuni ya kujisajili kwenye huduma zetu za tovuti, arifa za barua pepe na/au majarida.
- Maelezo mengine yoyote ambayo unachagua kutuma kwetu.
- Pale ambapo sheria inaturuhusu, wakati mwingine tunaweza kukusanya maelezo (kama namba yako ya simu) kutoka kikoa cha umma, moja kwa moja au kutoka kwa watu wengine, na tunaweza kuichanganya na maelezo tuliyo nayo kwa sasa.
3. Je, tunatumia kuki?
Tovuti ya Share Verified, kama tovuti nyingi, hutumia “kuki” ili kusaidia kubinafsisha uzoefu wako mtandaoni. Kuki ni faili ya ujumbe inayowekelewa na seva wa ukurasa wa wavuti kwenye diski yako ya kuhifadhi data. Kuki haziwezi kutumiwa kuendesha programu au kuwasilisha virusi katika kompyuta yako. Kuki hupeanwa kwako kwa njia spesheli, na zinaweza kusomwa tu na seva wa wavuti katika kikoa kilichotoa kuki kwako.
Huwa tunatumia Google Analytics ili kuchanganua matumizi ya tovuti hii. Google Analytics hutoa takwimu na maelezo mengine kuhusu matumizi ya tovuti kwa njia ya kuki, ambazo huhifadhiwa kwenye kompyuta za watumiaji. Maelezo yanayotolewa kuhusiana na tovuti yetu hutumiwa kuunda ripoti kuhusu matumizi ya tovuti. Google itahifadhi maelezo haya. Sera ya faragha ya Google inapatikana hapa. Watoa huduma za malipo/matangazo pia wanaweza kukutumia kuki.
Una uwezo wa kukubali au kukataa kuki. Vivinjari vingi vya wavuti hukubali kuki kiotomatiki, lakini kwa kawaida unaweza kubadilisha mipangilio ya kivinjari chako ili kukataa kuki ikiwa unapendelea. Ikiwa utachagua kukataa kuki, unaweza kukosa uwezo wa kupata uzoefu kamili wa vipengee vya mwingiliano wa huduma za createrefresh.eu au tovuti zingine unazotembelea.
Unaweza kujiondoa kwenye ukusanyaji data unaolenga matangazo hapa: http://www.aboutads.info/choices
4. Je, tutatumia data yako ya kibinafsi kwa njia gani?
Data ya kibinafsi inayotumwa kwenye tovuti hii itatumiwa kwa madhumuni yaliyoelezwa kwenye sera hii ya faragha au katika sehemu husika za tovuti. Tunaweza kutumia maelezo yako ya kibinafsi ili:
- Kusimamia tovuti;
- Kuboresha uzoefu wako wa kutumia mtandao kupitia kubinafsishwa kwa tovuti;
- Kuwezesha kupatikana kwa matumizi yako ya huduma kwenye tovuti;
- Kukutumia mawasiliano ya jumla (yasiyo ya uuzaji);
- Kukutumia arifa za barua pepe ambazo umeziomba hasa;
- Kukutumia mawasiliano ya uuzaji yanayohusiana na Verified na kampeni zetu, ambazo tunadhania kuwa zinaweza kuwa za maslahi bora kwako;
- Kufanya utafiti kuhusu athari za kampeni zetu;
- Kukuonyesha matangazo yanayolenga mitandao ya kijamii.
- Kutoa maelezo kuhusu watumiaji kwa njia ya takwimu kwa watu wengine – lakini maelezo haya hayatatumiwa kutambulisha mtumiaji yeyote binafsi;
- Kushughulikia maswali na malalamishi yanayohusiana na tovuti ambayo yanatolewa na au kukuhusu wewe;
- Kutoa uwasilishaji wa kesi za rufaa kwa watu wengine, ambapo umesaini rufaa, na mtu mwingine ndio lengo la kampeni ambayo rufaa inahusiana nayo.
- Ambapo unawasilisha maelezo ya kibinafsi ili kuchapishwa kwenye tovuti yetu, tutachapisha na tutatumia maelezo kwa njia nyingine ambayo bado ni kulingana na leseni unayotupatia.
Mbali na hali iliyowekwa katika sera hii, hatutauza, kukodisha au kushiriki data yako ya kibinafsi na mashirika ya watu wengine. Hata hivyo tunaweza kufichua maelezo yako kwa wasambazaji na washirika wa nje ili kutoa huduma fulani. Washirika na wasambazaji wote watakaguliwa ili kuhakikisha kuwa wanazingatia sheria na mahali ambapo mikataba ya data na makubaliano ya usiri yatakuwepo.
5. Je, data yangu itahifadhiwa wapi?
Maelezo yako yatahifadhiwa katika kompyuta zilizoko nchini Marekani. Ikiwa utawasilisha maelezo yako yanayokutambulisha kibinafsi kutoka ndani ya EU, maelezo hayo yatahamishwa nje ya EU hadi kompyuta zilizoko ndani ya Marekani. Tume ya Ulaya imekagua usalama wa faragha katika nchi kote ulimwenguni.
6. Je, utahifadhi data yangu kwa muda gani?
Tutahifadhi maelezo yako isipokuwa na hadi mojawapo wa hali hizi mbili zifikiwe:
- Purpose Global PBC iache kuwa shirika la kisheria
- Uondoe idhini yako ya matumizi na uhifadhi wa maelezo yako
7. Je, ninaweza kujua maelezo yale mlio nayo kwa njia gani?
Kwa wakati wowote, una haki ya kuomba nakala ya maelezo yako kutoka kwetu. Una haki ya kurekebisha makosa katika maelezo haya kwa wakati wowote. Tafadhali wasiliana na hello@shareverified.com kwa ombi lolote.
8. Marekebisho ya sera
Tunaweza kusasisha sera hii ya faragha mara kwa mara kupitia kuchapisha toleo jipya kwenye tovuti yetu. Unapaswa kuangalia ukurasa huu mara kwa mara ili uhakikishe kwamba unafurahia mabadiliko yoyote. Pia tunaweza kukujulisha kuhusu mabadiliko ya sera yetu ya faragha kwa njia ya barua pepe.
9. Tovuti za watu wengine
Tovuti hii ina viungo vya tovuti zingine. Hatuwajibikii sera za faragha au utendakazi wa tovuti za watu wengine.
10. Unajiondoa
Una haki ya kuondoa idhini yako ya matumizi na uhifadhi wa data yako wakati wowote. Tafadhali wasiliana na hello@shareverified.com kisha utujulishe, na tutafuta maelezo yako kutoka kwenye mifumo yetu na tukuthibitishie hili kwa njia ya kuandika.
11. Malalamishi
Ikiwa hufurahishwi na jinsi tunafanya kazi na data yako, tafadhali wasiliana nasi kupitia hello@shareverified.com kisha utujulishe. Ikiwa hatuwezi kutatua malalamishi yako kwa njia inayokuridhisha, una haki ya kuanzisha kesi rasmi ya malalamishi kuhusu vile tunafanya kazi na data yako kupitia mamlaka husika ya usimamizi chini ya Sheria ya Jumla ya Ulinzi wa Data (GDPR) katika EU:
Ofisi ya Kamishna wa Maelezo
Water Lane, Wycliffe House
Wilmslow – Cheshire SK9 5AF
Simu +44 1625 545 745
Barua pepe: international.team@ico.org.uk
Tovuti: https://ico.org.uk